Ngoma Mpya Kutoka Tanzania Wiki Hii

Image Source: Online 

Writer: Charles Maganga 

Mwezi February bila shaka umekuwa ni wakati bora sana kwa mashabiki wa Bongo Fleva ambao kwa mara nyingine wamepokea ngoma mpya kutoka kwa wasanii wanaowapenda. 

Kutoka kwa wasanii kama Ibraah, Maua Sama, Platform na wengineo wengi, hizi hapa ni ngoma mpya kutoka Tanzania kwa wiki hii: 

Dharau - Ibraah Ft Harmonize 

"Dharau" ni ngoma mpya ambayo Ibraah amemshirikisha Harmonize ambayo ndani yake Ibraah ametumia vionjo vya Bongo Fleva na Zouk kufikisha ujumbe kwa mpenzi wake kuwa hapendi dharau. Hii ni collabo ya tano baina ya wawili hao. 

Zamani - Maua Sama 

Kwenye “Zamani” ngoma yenye vionjo vya RnB na Bongo Flava, Maua Sama anamuomba mpenzi wake amrudishe miaka ya nyuma huku akikumbusha nyakati nzuri ambazo walishawahi kupitia.

 

Number One - Billnass Ft Mbosso 

Utapenda namna ambavyo sauti tamu ya Baibuda kutoka kwa Mbosso ilivyoshabihiana vizuri na michano laini ya Billnass kwenye ngoma hii ya kuitwa Number One ambayo ni ngoma ya kwanza kutoka kwa Billnass kwa mwaka huu. 

Body - Vanillah Ft Tommy Flavour 

Vijana kutokea Kings Music, Vanillah pamoja na Tommy Flavour wameungana pamoja kwenye Body, ngoma kali ya mapenzi ambayo ndani yake Vanillah na Tommy Flavour wanatoa sifa kedekede kwa mwenza wake. 

 

 

Leave your comment