Tegemea Albamu Mpya Mwaka Huu Kutoka Kwa Wasanii Hawa 3 Kutoka Tanzania

Image Source: Online

Writer: Charles Maganga 

Kwa miaka ya hivi karibuni wasanii kutoka Tanzania wamekuwa mistari wa mbele kuachia albamu za muziki kwa ajili ya kuburudisha mashabiki zao na kwa mwaka huu wa 2024 suala zima la albamu linaendelea kupamba moto. 

 

Wakati mwaka 2023, wasanii kama Tommy Flavour, Navy Kenzo na D Voice waliachia albamu zao, mwaka huu baadhi ya wasanii pia wamedokeza kuwa wako mbioni kuachia miradi yao mipya. 

Hawa hapa wasanii watatu ambao anatarajiwa kuachia albamu mwaka huu wa 2024: 

1.Zuchu

Tangu aachie EP yake ya I Am Zuchu mwaka 2020, Zuchu hajawahi kuachia “project” nyingine kubwa. 

Akiwa kwenye Insta live siku chache zilizopita wakati anatambulisha ngoma yake ya Zawadi, Zuchu alidokeza kuwa album yake iko tayari na kwamba anasubiri producer Lizer afanye “mixing and mastering” ili albamu hiyo iweze kutoka. 

 

2. Harmonize 

Tangu aanze muziki takriban miaka 9 iliyopita, kufikia sasa Harmonize ameshaachia album 4 na mwaka huu wa 2024, CEO huyo wa Konde Gang amedokeza kuwa yuko mbioni kuachia albamu yake ya 5. 

Kama Harmonize ataachia albamu nyingine ndani ya mwaka huu kama alivyoahidi basi atakuwa ni miongoni mwa wasanii kutoka Tanzania wenye albamu nyingi zaidi. 

3. Country Wizzy 

CEO wa I AM Music, Wizzy ameachia albamu moja tu ya kuitwa Yule Boy tangu aanze rasmi muziki miaka takriban 13 iliyopita.

Mapema wiki hii, Wizzy alidokeza kuhusu ujio wa albamu yake kupitia ukurasa wake wa Instagram baada ya kuandika “Sec album 80% done” hivyo kuchagiza mashabiki kushuku kuwa huenda Wizzy yuko mbioni kuachia albamu mwaka huu. 

 

 

Leave your comment