Ngoma Zinazofanya Vizuri Tanzania Wiki Hii

By Charles Maganga

Kutoka nchini Tanzania, wasanii wameendelea kuachia kazi kali ambazo mashabiki wameendelea kuzitazama na kusikiliza kupitia YouTube na hizi ni baadhi ya ngoma hizo ambazo zinafanya vizuri kwa wiki hii. 

 

Kutoka kwa wasanii kama Diamond Platnumz, Nandy na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma zinazofanya vizuri YouTube kwa wiki hii: 

 

1.Mapoz - Diamond Platnumz Ft Mr Blue & Jay Melody 

Baada ya siku takriban 12 hatimaye ngoma ya Mapoz kutoka kwa Diamond Platnumz imeshika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya ngoma zinazofanya vizuri YouTube nchini Tanzania. Ngoma hii kali ya mapenzi imetayarishwa na S2kizzy na imepokelewa vyema na mashabiki. 

https://youtu.be/M1dUTxVXS5Q?si=L0tzbYiIAeI2T00G

 

2. Dah! - Nandy Ft Ali Kiba 

Nandy na Ali Kiba wanaokutana kwa mara nyingine kwenye Dah! ngoma kali ya mapenzi ambayo kwa siku 10 mfululizo ilinga’nga’nia nafasi ya kwanza kwenye mtandao wa YouTube 

https://youtu.be/Oio_zNm9rxM?si=SpBx8ST2sLoMh8bb

3. I Made It - Harmonize Ft Bobby Shmurda & Bien

Bila shaka wapambanaji wote wameipenda ngoma ya I Made It kutoka kwa Harmonize na ndio maana tangu kuachia kwake wimbo huu umekuwa ukifanya vizuri sana na kwa wiki hii umeshika nafasi ya tatu. 

https://youtu.be/bPnOXwIzSFs?si=it4NB3ybmq81fHWt

 

4. Zawadi - Zuchu Ft Dadiposlim 

Kwenye ngoma yake mpya ya kuitwa Zawadi ambayo Zuchu aliiachia siku ya Valentine Day, msanii huyo kutokea WCB Wasafi ametunga mashahiri safi kusikia mapenzi na bila shaka wapendanao wote walipenda ngoma hii na kufanya kuwa ngoma pendwa kwao. 

https://youtu.be/nqxrYkKei0E?si=6foVSNuDhR_97II_

 

5. Umechelewa - Mbosso 

Kama kawaida yake, Mbosso ameweka uhalisia wa hali ya juu pamoja kucheza uhusika wa aina yake kwenye video yake mpya ya Umechelewa ambayo kwa wiki hii pia inafanya vizuri YouTube. 

https://youtu.be/gJA2riRXycA?si=2wCa10a505ZwWx7L

 

 

 

 

Leave your comment