Nyimbo Zinazotamba Wiki Hii - Tanzania
7 February 2024
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Stella Julius
Pakua Mixes Mpya za Valentines Ndani ya Mdundo.com
Wiki hii imeanza vizuri katika kiwanda cha Muziki wa Tanzania baada ya kushamirii kwa ngoma zenye zimeleta na kuibua ushabiki na kazi ya Muziki zenye ubora wa hali ya juu.Zifuatazo ni ngoma ambazo zinatamba zaidi nchini Tanzania.
Nandy ft Ally Kiba - Daah!
Mmiliki wa lebo ya The African princes Nandy amefanikiwa kuachia remix ya ngoma yake ya Daah! ambayo pia amemshirikisha nguli wa Muziki wa bongo fleva Ali Kiba. Kwa sasa ngoma hiyo Ina takribani siku tatu tangu kuachiwa kwake na kupendea zaidi. Daah imeongozwa na Director Folex huku audio ikipita katika mikono ya S2kizzy
Diamond Platnumz ft Mr Blue & Jay Melody - Mapoz
Baada ya miaka 14 kupita Mapoz imerejea Tena huku ikiwa ni Moja kati ya ngoma zilizopendwa ambazo pia zimerejea kwa kishindo.
Mbali na ukubwa wa ngoma ya Mapoz , hii ni kolabo iliyosubiriwa kwa hamu kati ya Diamond pamoja na Jay Melody.
Dulla Makabila - Furaha
Kinara wa Muziki wa singeli nchini Tanzania Dulla Makabila ameachia ngoma yake ya Furahi ikiwa ni ngoma iliyopendwa kwa mwaka huu katika singeli kutokana na stori ya ngoma hiyo. Ngoma hiyo yenye utata umevutia wengi kutokana na uandishi wake uliosemekana kumlenga aliyekuwa mke wake. Furahi ni singeli iliyofanya na Producer Goodmaster wa nchini Tanzania.
Harmonize ft Bobby Shmurda & Bien
Katika harakati za kuipekeka bongo fleva kimataifa zaidi, mwanamuziki Harmonize ameamua kuwakutanisha nyota wa Muziki wa Rap Bobby Shmurda kutokea Marekan pamoja na Bien wa nchini Kenya. Wimbo wa I made it umefanya na producer Sign_beats.
Ney wa mitego - Wako huko
Moja kati ya wasanii ambazo wanasifika kwa kuandika nyimbo zenye ukosoaji ni mwanamuziki Ney wa mitego. Katika wimbo wa Wapi huko Ney ameelezea juu ya nchi au sehemu ambayo imekuwa ikitoa vipaumbele katika vitu visivyo na maana na kiacha mambo au majukumu ya muhimu
Katika upande wa beats ngoma hiyo imepita Touchez sound huku video ikifanywa na Mr. Zizi.
Leave your comment