AUDIOBOOK: Sikiliza Riwaya Kamili "Kimo" yake Fredrick Bundala Ndani Ya Mdundo

[Image Source: Instagram]

Pakua Mixes Mpya Kila Siku Ndani Ya Mdundo

Kimo anajikuta njia panda, kuufuata moyo wake au kumridhisha baba yake. Anaamua kucheza kamari ya maisha kwa kwenda kinyume na kile baba yake alitaka awe. Anajikuta akifukuzwa nyumbani kwao na kumlazimu kuanza maisha ya ghetto, ambayo hajawahi kuyapitia. Kwenye maisha ya upangaji anakutana na Munerah, anayependana naye lakini penzi lao halidumu baada ya Munerah kulazimishwa kuolewa Oman.

Wanaachana wakiwa bado wanapendana sana. Kimo anakutana na Jamillah, msichana maarufu na mrembo kupita kiasi aliyekuwa akimpenda mno hadi kubandika picha zake ukutani. Anajikuta akipigania vitu viwili vikubwa, kutafuta mafanikio kumthibitishia baba yake kuwa kwa kufuata moyo yake hakuwa anapotea na kuliwinda penzi la Jamillah, msichana wa ndoto yake mikononi mwa Branx.

Sikiliza Simulizi hii ya Kimo hapa ndani ya Mdundo.com

Leave your comment