Saba Saba Vibe: Tuadhimishe aina Tofauti Za Mziki kutoka Tanzania Ndani Ya Mdundo



[Picha: Mdundo.com]

Mwandishi: Branice Nafula

Pakua Mixes Mpya Kila Siku Ndani Ya Mdundo

Katika juhudi za kuhamasisha jamii kuhusu ushirikiano wa Mdundo, jukwaa la muziki la kidijitali linaloongoza, na Vodacom Tanzania, kampuni kubwa ya mawasiliano ya simu nchini, wakijiandaa kuleta sherehe ya Saba Saba,tunakupa fursa ya kujua baadhi ya aina tofauti za Mziki kutoka Tanzania.

Mziki kutoka Tanzania unaendelea kukua kila kukicha huku watu wengi nje ya Tanzania wakijua kuhusu aina moja tu maarufu- Bongo Flava.

Hivyo hapa tukisubiria kwa hamu shughuli nzima ya Saba Saba mnamo tarehe 7 Julai 2023, kule Dar Es Salaam, jipe fursa ya kukagua na kupakua mixes kali na hata nyimbo za aina tofauti za mziki ndani ya Mdundo.com

Bongo Flava
Bongo Flava ndio aina ya mziki unaokubaliwa zaidi kutoka Tanzania kufikia sasa.Kupitia Mziki huu viajan wengi kutoka Tanzania wanatengeza kipato chao kupitia uimbaji, uandishi, kuwa waandalizi wa
mziki(Producer) na kaiz zingine mingi. Mziki huu ulichupuka miaka ya 90 huku wasanii waliokuwepo miaka ile wakiwaandalia wa kisasa upeo wa kujipatia kipato. Kufikia sasa wasanii wanaokubalika ulimwenguni kutoka bongo kupitia bongo Flava ni kama vile Diamond Platnumz, Alikiba, Lady Jay Dee, Ray C na wengineo.Hii leo wasanii wa bongo wanaokubaliwa sana na mashabiki ni kama vile Mbosso,Marioo, Mabantu


Taarab
Muziki wa Taarab ni miongoni mwa aina nyingi katika muziki wa Tanzania ambao umeathiriwa zaidi na mitindo ya kitamaduni ya Kiafrika. Muziki wa Taarab ni muunganiko wa nyimbo za Kiswahili za kabla ya Uislamu zilizoimbwa kwa mtindo wa ushairi wenye mahadhi, uliokolezwa na nyimbo za kiarabu. Ni aina ya sanaa ya kusisimua sana, na inajulikana sana hasa na wanawake.Mziki huu pia ni maarufu kwenye mtandao wa Mdundo.

Singeli

Muziki wa Singeli ni toleo la Tanzania la muziki wa dansi wa kielektroniki ulioibuka katikati ya miaka ya 2000. Mtindo huu unachanganya midundo ya kasi na ushawishi wa muziki kutoka kwa aina kongwe za Kitanzania kama vile Taarab, Mchiriku, Segere, na Bongo Flava. Ala, sampuli, na sauti mara nyingi huhamishwa juu, na kuongeza mdundo wa kasi.

Qaswida
Huu ni mziki wa dini ya Kiislamu. Ni Mziki wa  kuwahamasisha watu wengine katika kumtukuza Mungu. Qaswida ni muziki wa kiroho na utulivu.Na katika mtandao wa Mdundo mziki huu unapatika kwa urahisi sana. Upakue hapa!

Leave your comment