Country Wizzy Atambulisha Kundi Jipya La Hip Hop “Freshboys” 


Picha Instagram

Imeandikwa na Charles Maganga

Moja ya vitu vinavyozungumziwa sana nchini Tanzania kwa sasa ni pamoja na kundi jipya la muziki wa Hip Hop nchini la kuitwa Freshboys, kundi ambalo lilitambulishwa rasmi siku chache zilizopita. 

Rapa Country Wizzy hivi karibuni kupitia lebo yake ya “I AM MUSIC” alitambulisha kundi hilo ambalo linaundwa na vijana wanne wenye vipaji vya aina yake ambao ni T Boy Mill, 10k Degreez, 6ix TooGood  pamoja na Gran Jeez. 

Sambamba na utambulisho huo wasanii hao pia wameachia ngoma mpya ya kuitwa “Manaake Nini” ambayo inazungumzia mambo mbalimbali kuhusu maisha na tabia za watu kwa ujumla wake. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Country Wizzy aliwashukuru wote walioshiriki mpaka kuwatambulisha Freshboys kwenye kiwanda cha muziki na kuongeza kwa kuwaomba mashabiki waweze kuwaunga mkono vijana hao wapya kabisa kwenye kiwanda cha muziki Tanzania. 

Leave your comment