Baada Ya “Nobody” Darassa Adokeza Ngoma Mpya 


Picha: Instagram

Imeandikwa na Charles Maganga

Kama uliipenda ngoma ya Darassa ya kuitwa “Nobody” iliyotoka mapema mwaka huu basi habari njema ni kwamba rapa huyo amedokeza ujio wake mpya kabisa baada ya kutoa kionjo cha ngoma mpya. 

Kwa mwaka 2023 Darassa ameachia ngoma tatu ambazo ni “Dead Zone” “Mind Your Business” na “Nobody” ambayo kamshirikisha Bien kutokea huko nchini Kenya na tangu hapo mashabiki wamekuwa wakisubiri kwa hamu ujio mpya wa rapa huyo ambaye anajulikana kwa uwezo wake wa kutoa “Hit Songs” 

Kupiti ukurasa wake Instagram, Darassa aliweka kionjo cha ngoma yake mpya ambapo rapa huyo alionekana katika video akiwa anaimba ngoma hiyo kisha kuisindikiza na hashtag ya “Slow But Sure” ambayo imeshukiwa kuwa ndio jina la wimbo huo. 

Kwenye chapisho hilo la Instagram, watu mbalimbali maarufu ikiwemo S2kizzy, Platform, Adam Mchomvu, Diamond Platnumz na wengineo walionekana kusubiri kwa hamu ngoma hiyo mpya kutoka kwa Darassa. 

Leave your comment