Zifahamu Collabo 5 Za Kimataifa Kutoka Zuchu 

Picha: Instagram
Mwandishi:
Charles Maganga


Tangu kutangazwa kwake kuwa msanii wa WCB mnamo mwaka 2020, Zuchu amekuwa mstari wa mbele katika kuipeleka Bongo Fleva kimataifa na moja kati ya silaha anazozitumia mwanamuziki huyo ni pamoja na collabo wasanii wengine wa Afrika. 

Akiwa na miaka takriban mitatu tu kwenye kiwanda cha muziki, Zuchu ameweza kufanya na wasanii kutokea Nigeria, Uganda na hata huko chini Congo na wafuatao ni wasanii wa kimataifa ambao wameshawahi kufanya kazi na msanii Zuchu. 

Joeboy - Nobody 

Mwaka 2020, Zuchu alianza safari yake ya kwenda kimataifa na “Nobody” ngoma aliyomshirikisha msanii kutokea Nigeria, Joeboy. “Nobody” ilikuwa ni ngoma pendwa ambayo ilitikisa kila pande ya Afrika pindi ilipoachiwa. 
https://youtu.be/04Roh3SDyN0

Sere - Olakira 

Kwenye ngoma hii “Zuchu” alishirikishwa na msanii kutokea nchini Nigeria wa kuitwa Olakira. Zuchu alinogesha ngoma hii kwa sauti ya nzuri pamoja na mashahiri yake ambayo bila shaka yalikonga mashabiki wengi. 
https://youtu.be/wht8D5mekJ8

Upendo - Spice Diana

Kwenye wimbo huu, Zuchu alipata nafasi ya kutambulisha zaidi muziki wake huko nchini Uganda. Kwenye “Upendo” Spice Diana alionesha ufundi wake wa kuimba Kiswahili fasaha huku Zuchu akipamna ngoma hiyo kwa sauti yake mujarab
https://youtu.be/n9oTjjfkXJA

Love - Adekunle Gold 

Love ni moja kati ya ngoma kali kabisa kwa za mapenzi ambazo Zuchu alishawahi kufanya na utamu wa ngoma hiyo ulinogeshwa zaidi na Adekunle Gold kutokea nchini Nigeria ambaye bila shaka aliweza kukaimu vyema nafasi yake katika wimbo huo. 
https://youtu.be/ECRf_qsQ8jY

Kiss - Innos B 

Chemistry au ushirikiano wa Zuchu na Innos B kwenye wimbo huu unaonesha wazi kuwa Zuchu ana uwezo mkubwa wa kuimba na kufanya aina yoyote ya muziki. “Kiss” bila shaka imeweka msingi mzuri kwa ajili ya Zuchu kutambulika zaidi huko nchini Congo. 
https://youtu.be/vr9Vt7htryU

Leave your comment