Muziki Mpya Tanzania: Wasanii Nguli Ambao Hawajatoa Albamu


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Moja kati ya vitu ambavyo vinamheshimisha na kuonesha ukubwa wa msanii basi bila shaka ni albamu za muziki na kwenye kiwanda cha muziki Tanzania ambacho kimejaa wasanii wengi wakubwa, bado kuna baadhi ya wasanii ambao hawajaachia albamu hata moja. 

Katika makala hii tunaenda kuangazia, orodha ya wasanii wakubwa Tanzania ambao kufikia sasa bado hawajaachia albamu zao za muziki: 

Jay Melody 

Jay Melody ana ngoma kali sana ikiwemo “Huba Hulu” “Nakupenda” “Sawa” na nyinginezo nyingi na pamoja na kuwa silaha nyingi kwenye ghala lake la muziki lakini bado fundi huyu wa Bongo Fleva hajaachia albamu yake rasmi. 

Zuchu 

Mshindi huyu wa tuzo 5 kwenye Tanzania Music Awards 2023 bado hajaachia albamu rasmi kwa ajili ya mashabiki zake. Ukiweka kando EP yake ya “I Am Zuchu” ambayo ilimtambulisha vyema kwa muda mrefu sasa mashabiki wamekuwa wakisubiri albamu mpya kutoka kwa staa huyu 

Billnass

Linapokuja suala la kutengeneza “Hit” Billnass ndiye mtaalamu haswa lakini bado fundi huyu wa Hiphop Tanzania hajaachia albamu. 

Billnass anatamba na ngoma tofauti kama “Chaf Pozi” “Mazoea” “Mafioso” na “Puuh” ya mwaka 2022 ambayo ilifanya vizuri sana 

Maua Sama 

Maua Sama ameshafanya kila kitu kwenye Bongo Fleva. Ameshashinda tuzo, ana hits za kutosha, ana collabo za kimataifa na mengineyo mengi lakini kitu pekee ambacho mashabiki wanakosa kutoka kwake ni album. 

Ukiweka kando EP yake ya Sinema, staa huyo wa Bongo Fleva hivi karibuni alidokeza kuachia albamu yake ya kuitwa “Love Waves” ambayo bado haijatoka. 

Tommy Flavour 

Mwanzoni mwa mwaka huu Tommy Flavour alikosa mashabiki zake na “Nakuja” ngoma ambayo alimshirikisha Marioo na utamu wa ngoma hiyo bila shaka ulitakiwa uzue mjadala kuhusu ni lini haswa Tommy ataachia albamu yake. 

Kwa muda mrefu sasa Tommy Flavour amekuwa alidokeza kuhusu ujio wa albamu yake ya “Heir To The Throne” lakini kufikia sasa bado albamu hiyo haijaingia sokoni.

Leave your comment