Ngoma Mpya Tanzania: Jux Afichua DJ Ally B Kushiriki Kwenye Ngoma Yake


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 

DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Kama kuna ngoma ambayo kwa sasa inasumbua kwenye klabu na mitandao ya kijamii basi bila shaka ni ngoma ya kwake Jux ya kuitwa “Shuga Daddy” ambayo amefanya na DJ Tarico pamoja  G Nako. 

Sasa hivi karibuni Juma Jux amefichua kuwa DJ maarufu kwa sasa nchini Tanzania, DJ Ally B pia  amehusika katika kuandaa ngoma hiyo yenye miondoko ya Amapiano. 

DJ Ally B ni moja kati ya Ma-DJ bora na maarufu  kutoka Tanzania kwa sasa ambapo hivi karibuni alishinda tuzo ya DJ Bora Wa Kiume Wa Mwaka kwenye Tuzo Za Tanzania Music Awards 2023. 

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jux aliweka video inayomuonesha DJ Ally B akiwa anaweka anarekodi studio ambapo DJ huyo anayetokea mkoani Moshi alionekana akiwa anapuga miluzi na kuweka vionjo vyake kwenye wimbo huo. 

“Thank you so much my brother DJ Ally B  Kama ulikuwa haujui kwenye Shuga Daddy  nakujuza. MIRUZII imepigwa na BINGWA wa miruzi Nchini Dokta DJ Ally B” aliandika msanii huyo. 

Leave your comment