Hatimaye Rayvanny Aachia FLOWERS III Tanzania


[Picha: Instagram]

Mwandishi-Charles Maganga 


DOWNLOAD LATEST BONGO MUSIC MP3

Mwanamuziki kutoka Tanzania, Rayvanny hatimaye ameachia EP yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu sana na mashabiki ya kuitwa Flowers III

Flowers III ni EP ya tatu katika mtiririko wa Flowers EP kutoka kwa mshindi huyo wa tuzo  za BET. Flowers ya kwanza ilitoka mwaka 2020 huku Flowers II ikiwa imeachiwa mwaka 2022 ambapo Rayvanny aliwashirikisha wasanii kama Zuchu, Ray C na Marioo. 

Kwenye Flowers III Rayvanny ametengeneza ngoma 9 ambapo 3 kati ya hizo ambazo ni “Forever” “One Day Yes” na “Mwambieni” tayari zimeshatoka. Aidha kwenye EP hii Rayvanny ameshirikisha wasanii tofauti tofauti tofauti ikiwemo Phina, Jay Melody, Mac Voice na Bahati kutoka Kenya. 

Ikumbukwe kuwa kufikia sasa Rayvanny ana jumla ya EP 5 pamoja na albamu moja ambayo ni Sounds From Africa ya mwaka 2021. 

Leave your comment

Top stories

More News