Nyimbo Mpya: Platform Aungana Na Marioo Kwenye “Ananipenda”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Fundi wa muziki wa Bongo Fleva Platform ameamua kwa mara nyingine kuburudisha mashabiki zake baada ya kuachia “Ananipenda” ngoma ambayo amefanya na Marioo.

Ananipenda ni ngoma ya taru  kutoka kwa Platform kwa mwaka huu baada ya kuachia ngoma nyingine mbili ambazo ni “Wivu” pamoja na “Mapepe”

Ananipenda ni ngoma ambayo Platform na Marioo wanasimulia namna ambavyo wanapendwa na wenza wao huku wakihadithia jinsi ambavyo mapenzi yana nguvu na inayokuja kutokana raha ya kupendwa. Platform na Marioo pia walishashirikiana kwenye ngoma ya “Fall” ya mwaka 2022. 

Abbah Process ndiye amehusika kutayarisha ngoma hii ambayo inatarajiwa kufanya vizuri nchini Tanzania. Ngoma nyingine kutoka kwa Abbah ambazo zimeingia sokoni mwaka huu ni pamoja na “Nakuja” ya Tommy Flavour na Marioo pamoja na “Salama” ya Rose Muhando na Christina Shusho.

https://www.youtube.com/watch?v=1OHq1dc6YYo

Leave your comment

Top stories

More News