Vanessa Mdee Alivyobadilisha Kiwanda Cha Muziki Tanzania

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Imeshapita takriban miaka 3 tangu Vanessa Mdee atangaze kupumzika kufanya muziki na tangu kuondoka kwake kumekuwa na pengo ambalo bado hajapatikana wa kuliziba.

Vanessa Mdee alikuwa ni vitu vingi kwa watu wengi. Alianza kama VJ wa MTV Base Africa, kisha akahamia kwenye utangazaji wa vipindi vya TV ikiwemo Bongo Star Search na mwaka 2013 ndipo aliingia rasmi kwenye muziki kwa kuachia “Closer” ngoma ambayo ilishinda tuzo ya wimbo bora wa RnB kwenye tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Awards.

Ndani ya miaka takriban 7 aliyohudumu kwenye muziki, Vanessa Mdee ameacha alama ambayo haijafutika. Ukizungumza na wasanii kama Phina, Zuchu, Abigail Chams, Anjella na wengineo wengi watakubali kwamba Vanessa alikuwa na atakuwa “Legend” siku zote.

Hivi Ndivyo Malkia Wa “Money Mondays” Alivyobadilisha Kiwanda Cha Muziki Tanzania:

Gharama Za Video

Vanessa Mdee ni moja ya wasanii wa mwanzo kabisa kumwaga pesa nyingi sana katika kutengeneza video kali. Mathalani Video yake ya “Never Ever” katika moja ya mahojiano, Vanessa alidokeza kutumia Dola 20,000 mpaka kuikamilisha.

Video nyingi za Vanessa Mdee hazikutengenezwa Tanzania kwani alipendelea kufanya video Kenya na Afrika Kusini ili kuongeza “Fanbase”.  Baadhi ya Video hizo ni pamoja na “Cash Madam”, “Nobody But Me” Na “Hawajui”.

 

Collabo Za Kimataifa

Ukimuweka kando Diamond Platnumz, Vanessa alikuwa ni moja ya wasanii waliokuwa na collabo nyingi za kimataifa kutoka Kenya, Nigeria, Ghana na kwingineko.

Vanessa alihusika katika “Movement Ya Bongo Fleva To The World” na mpaka anapumzika alikuwa ameshafanya kazi na wasanii kama Reekado Banks, Mr P, Cassper Nyovest, Mohombi na wengineo wengi.

Kufungua Lebo

Vanessa Mdee ni moja ya wasanii wachache Afrika ambao walikuwa na uthubutu wa kufungua lebo.

Mdee Music ilikuwa ni nyumbani kwa Mimi Mars na rapa Brian Simba na kupitia lebo hii Vanessa alikuwa tayari kwa ajili ya kutengeneza vipaji vingine vipya kwenye kiwanda cha music Tanzanian

Ushawishi Wa Kimataifa

Vanessa Mdee alikuwa ni watu katika tasnia ya burudani Afrika. Vanessa Mdee alikuwa ni moja ya wasanii wachache Afrika ambao walipata dili la kusaini na Universal Music Group kutokea Marekani.

Vanessa pia alikuwa ni mtangazaji na VJ  wa kituo cha MTV Base na pia alikuwa ni moja ya waamuzi (judge) kwenye shindano la East Africa Got Talent.

Leave your comment