Nyimbo Zinazotamba Tanzania Wiki Hii
31 March 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Bongo Fleva inazidi kuchangamka kutokana na ushindani ambao upo baina ya wasanii hasa katika suala zima la kutoa ngoma kali na katika wiki hii ya mwisho ya mwezi Machi zifahamu ngoma ambazo zimeteka na kufanya zaidi hapa nchini Tanzania kwenye mtandao wa Youtube
Kutoka kwa Harmonize mpaka kwa Darassa zifahamu ngoma kali zinazofanya vizuri hapa Tanzania kwenye mtandao wa Youtube
Single Again - Harmonize
Ufundi wa Director Kenny umeonekana barabara kwenye video hii ya Harmonize ya kuitwa “Single Again” ambayo kufikia sasa imeshakusanya watazamaji takriban Milioni 1.2 Youtube tangu kuachiwa kwake
Jua Lile - Nacha Ft Stamina
Ngoma hii “Jua Lile” inaweza kusikilizwa na yeyote kwani ndani ya mkwaju huu Nacha na Stamina wamepiga stori nyingi sana kuhusu maisha ya kila siku, muziki wa Tanzania na mambo mengine nengi sana.
Napambana - Zuchu
Ngoma hii ya Zuchu imeendelea kupambania kombe ili kuweza kuendelea kushika nafasi za juu kwenye Youtube. Tangu kuachiwa kwake “Napambana” ya Zuchu imeshakusanya watazamaji Milioni 2.7 Youtube
Nani? - Abigail Chams Ft Marioo
Kwenye Amapiano hii mujarab, Abigail Chams na Marioo wanasifiana, wanapongezana na kutupiana maneno matamu ili tu kunogesha mahusiano yao. Wengi wamependa ngoma hii kutokana na beat kali na muingiliano mzuri wa sauti baina ya wawili hawa
Mind Your Business - Darassa
Ngoma ya Darassa “Mind Your Business” inazidi kupepea. Kwenye ngoma hii utapenda mashahiri mazuri kutoka kwa Darassa pamoja na video fupi na isiyoboa ambayo ndani yake anaonekana DJ maarufu kutoka Tanzania, DJ Ally B
Leave your comment