Harmonize Afichua Siri Ya Ngoma Za Jay Melody Kufanya Vizuri

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwanamuziki nguli kutoka Tanzania ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya “Single Again” Harmonize hivi karibuni ametoa mawazo yake kuhusu hasa nini kimepelekea ngoma za Jay Melody kuendelea kufanya vizuri.

Jay Melody kwa sasa anatamba na ngoma yake ya “Sawa” ambayo inafanya vizuri sana kwenye mitandao ya kusikiliza muziki pamoja na TikTok huku ngoma yake ya mwaka 2022 ya kuitwa “Nakupenda” ilikuwa ni moja ya ngoma bora kwa mwaka huo.

Kupitia ukurasa wake wa Instastory, Harmonize alisifia muziki wa Jay Melody kwa kusema kuwa Jay Melody anatengeneza muziki ambao wanawake wengi wa kizazi hiki wanapenda na kuongeza kuwa katika uandishi wake Jay Melody hatumii nguvu kabisa.

“ITS LIKE Jay Melody Anajua Kilichomo ndani Ya Kichwa Cha Kila Mwanamke Wa Generation Mpyaa. Kwahiyo Hata Mwamba Usipoelewa Watoto wazuri watakuelewesha

Hatumii Nguvu Kabisaa. Congrats Bro Keep that” aliandika Harmonize.

 

“Ikumbukwe kuwa Harmonize na Jay Melody hivi karibuni walitajwa kuwepo kwenye orodha ya nyimbo pendwa za Makamu Wa Rais Wa Marekani ambapo ambapo Single Again ya Harmonize na Sawa ya Jay Melody zilitajwa kwenye orodha hiyo”

Leave your comment