Cheq Bob Afichua Siri Mpaka Kusainiwa Na Rapa Young D
31 March 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Moja ya wasanii chipukizi wanaotamba Tanzania kwa kipindi hiki ni Cheq Bob ambaye kwa sasa amesainiwa kwenye lebo ya rapa Young Dee ya kuitwa Dream City.
Cheq Bob kwa sasa anatamba na ngoma yake ya Tattoo ambayo imetoka siku chache zilizopita.
Kulingana na Young Dee kupitia ujumbe aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, rapa huyo alimsifia Cheq Bob kwa kudokeza kuwa kutokana na ujio wa Cheq Bob kwa sasa Bongo Fleva imepata “zawadi” nyingine kubwa.
Akizungumza hivi karibuni Wasafi FM, Cheq Bob alidokeza kuwa Young D aliamua kumsaini kwa sababu aliona yeye ana kitu na kuongeza kuwa pamoja na kuaminiwa na Young Dee lakini hata yeye alikuwa bado hajajipata tofauti na sasa.
“Young D alikuwa anaona kuna kitu ninacho. Alikuwa anaona lakini nilikuwa bado sijajipata. Ndo maana nakwambia kipindi kile nilikuwa na-hustle sana ila sasa hivi freshi yaani na-enjoy” alizungumza Cheq Bob
Ikumbukwe kuwa ngoma ya Cheq Bob ya kuitwa “Tattoo” imepokelewa vyema na mashabiki na wadau wa muziki ambapo marapa wakubwa Tanzania kama Billnass na Darassa wameonekana kuvutiwa na ngoma yake hiyo.
Leave your comment