Killy Afunguka Kupewa Milioni 10 Na Konde Gang Ya Harmonize

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii kunako kiwanda cha Bongo Fleva, Killy hivi karibuni amefunguka kuhusu taarifa zilizoenea mtandaoni kuwa alipewa Milioni 10 za kitanzania ili aweze kuvunja mkataba na lebo kubwa ya muziki Tanzania, Konde Music Worlwide.

Ikumbukwe kuwa Killy aliondoka Konde Gang mwezi Oktoba mwaka jana ambapo yeye na Cheed walitangaza kuachana na lebo hiyo kubwa ambayo inamilikiwa na Harmonize.

Akiwa kwenye mahojiano na Clouds Digital hivi karibuni, Killy alikanusha kuchukua Milioni 10 ambapo alisema kuwa katika kumalizana na lebo hiyo alipewa machaguo mawili.

 La kwanza ni kupokea pesa kiasi cha Tsh Million 10 na kisha aachane na umiliki wa 100% wa hakimiliki ya nyimbo zake, ama asipewe pesa ili abaki na umiliki wa 100% wa hakimiliki ya nyimbo zake na yeye hakuchagua pesa akaamua kuchagua hakimiliki.

“Sikupewa Milioni 10. Kulikuwa na suggestions mbili wakupe Milioni 10 au wakupe hakimiliki zako mwenyewe umiliki asilimia 100. Mimi nilichagua kumiliki vitu vyangu mwenyewe asilimia mia. Sikuhitaji chochote” alizungumza Killy kwenye mahojiano hayo.

Leave your comment