Video Za Harmonize Zilizotazamwa Zaidi
28 March 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Nchini Tanzania, Harmonize ndiye msanii wa tatu, nyuma ya Diamond Platnumz na Rayvanny kwa kuwa na wafuasi (subscribers) wengi zaidi Youtube huku Chanel yake ikiwa imeshatazamwa takriban mara Milioni 878 kwenye mtandao huo.
Kupitia makala hii tunaenda kuzihesabu video 5 za muziki kutoka kwa Harmonize zilizotazamwa zaidi kwenye chaneli yake ya Youtube
Kwangaru Featuring Diamond Platnumz
Kwangaru ndio ngoma ya Harmonize iliyotazamwa zaidi Youtube ambapo kufikia sasa imeshakusanya watazamaji Milioni 102 kwenye mtandao wa Youtube. Video ya Kwangaru ilitoka mwaka 2018 na ilitayarishwa na Director Kenny
Happy Birthday
Happy Birthday ni moja kati ya ngoma maarufu sana kutoka kwa Harmonize na kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 41 kwenye mtandao wa Youtube.
Bado Featuring Diamond Platnumz
Bado ilikuwa ni video ya pili kutoka kwa Harmonize tangu kusainiwa WCB Wasafi na kutokana na stori ya video hii kuwa kali wengi walivutiwa na video hii ambayo kufikia sasa imeshatazamwa mara Milioni 36. Video ya Bado ilifanyika Afrika Kusini na iliongozwa na Nicklass.
Aiyola
Aiyola ndio ngoma na video iliyomtambulisha Harmonize kwenye uwanja wa Bongo Fleva na kufikia sasa video hii imeshatazamwa mara Milioni 28 kwenye mtandao wa Youtube
Magufuli
Kwenye ngoma hii, Harmonize alilenga kumpa sifa kedekede aliyekuwa Rais Wa Tanzania, John Pombe Magufuli na ili kufanya hivyo, Harmonize aliufanyia remix wimbo wa “Kwangaru” ambapo aliisindikiza ngoma hiyo na video kali ambayo kufikia sasa imeshakusanya views Milioni 28 Youtube.
Leave your comment