Mabantu Watambulisha “University Ep”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kundi la muziki kutoka Tanzania, Mabantu hivi karibuni wametambulisha EP yao mpya kabisa ya kuitwa University EP ambayo inatarajiwa kuwa mradi wao wa kwanza wa muziki tangu waanze muziki.

Ikumbukwe kuwa, Mabantu ambao ni muunganiko wa Muuh na Twaha wamekuwa kimya bila kutoa kazi yoyote kwa takriban miezi sita na mara ya mwisho kuachia kazi ilikuwa ni Septemba mwaka 2022 walipoachia mkwaju wao wa kuitwa Leo ambao wameshirikiana na Marioo.

Kupitia kurasa zao za Instagram Mabantu walidokeza kuhusu ujio wa EP hiyo ambapo, University EP inatarajiwa kuwa na ngoma 8 na kati ya hizo ni moja tu wameshirikisha msanii ambaye ni Baddest 47. Aidha EP hiyo imetayarishwa na Chiby pamoja na Gachi B.

University EP inatarajiwa kuingia sokoni kesho Tarehe 28 Machi 2023.

Leave your comment