Wasanii 5 Wa Kuwasikiliza Kipindi Hiki Cha Ramadhan
22 March 2023
Download FREE Ramadhan Mix on Mdundo.com
Kwa wengi muziki hasa ule wa aina Nasheed bila shaka umekuwa ni kiungo muhimu sana katika mwezi huu wa Ramadhan. Katika makala hii tunakuletea wasanii watano ambao muziki wao bila shaka utakufundisha mengi na kukuburudisha pia katika mwezi huu wa Ramadhan.
Afaaizu Luheta anajulikana kwa nyimbo kama “Aggash” , “Ewe Nafsi Kinai” na nyinginezo nyingi ambazo zimechagiza watu wengi kumfahamu na hivi karibuni aliweza kuwakosha wengi zaidi na wimbo wake mpya unaoitwa “Dont Ever Let Me Down”
Kutokea nchini Kenya, Brother Nassir ni moja ya waimbaji hodari sana ambae nyimbo zake sio tu kwamba zitakupa faraja lakini pia zitakuburudisha sana. Brother Nassir anafanya vizuri na nyimbo kama “Wangu Wa Halali” ambao ni wimbo maalum kwa ajili ya sherehe za harusi na hivi karibuni aliachia wimbo wake wa “Pepo Ya Dunia”
Bila shaka Yahaya Mohammed ni moja ya wasanii wanaostahili kupewa sikio hasa kipindi cha Ramadhani kwani nyimbo zake kama “Baba” “Alonipa” na “Usihofu” bila shaka zitakufundisha mengi usiyayojua na kukumbusha yale mema uliyosahau kuhusu dini na maisha kwa ujumla.
Mwimbaji huyu wa kuitwa Filyatul Iman ana kipaji kikubwa sana na kupitia nyimbo zake “Usihuzunike” , “Radhi Ya Mama” na “Karibu Ya Ramadhan” ambao ni wimbo maalum kwa ajili ya mwezi huu mtukufu basi bila shaka utajifunza na kupata mawaidha mengi mazuri kutoka kwake.
Team Brothers
Uzuri wa Team Brothers sio tu kwamba wana mashahiri mazuri lakini pia utapata burudani na mafunzo ya aina yake pindi wanapotumbuiza nyimbo mbalimbali. Baadhi ya nyimbo zao ni pamoja na “Assalam Aleykum” “Umoja” na nyinginezo nyingi.
Leave your comment