Skales wa Nigeria Ashangazwa na Wimbo wa Harmonize 'I’m Single'

Download FREE Mp3 Music by Skales on Mdundo.com

Msani kutokea nchini Nigeria, Skales ameonekana kushangazwa na kushtushwa bna mafanikio ya ngoma ya hivi karibuni ya Harmonize kupitia ngoma yake yake ya “Im Single” 

Skales ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake ya “Konibanje” ameoneshwa kuguswa na ngoma mpya ya “Single Again” ya kwake Harmonize. Ngoma ya “Single Again” ya Harmonize iliachiwa Februari 14 mwaka huu na tangu kuachiwa kwake imekuwa ni ngoma pendwa baina ya mashabiki. 

Kupitia ukurasa wake wa Instastory, Skales alichapisha video fupi ambayo inaonesha ngoma ya “Single Again” ikiwa imeshika nafasi ya 6 kwenye Chati za Shazam huko nchini Nigeria na kuandika “My Bro Harmonize Climbing This Naija Charts Lezz Go” 

Ikumbukwe kuwa Harmonize na Skales ni marafiki wa muda mrefu na kuna kipindi Skales alikuwa amesainiwa kwenye lebo hiyo ya Harmonize ya kuitwa Konde Music Worldwide.

Leave your comment

Top stories