Joh Makini Aachia EP Yake Ya 'Wave'

Download FREE Mp3 Music by Joh Makini

Msanii Joh Makini ameamua kupeperusha vyema bendera ya Muziki wa Hip Hop Tanzania na hii ni baada ya kuachia EP yake mpya kabisa ya kuitwa Wave 

Hii ni EP ya kwanza kutoka kwa Joh Makini tangu aanze muziki na ni mradi wake mkubwa wa kwanza wa muziki tangu ashiriki kwenye albamu ya “Air Weusi” ambayo iliingia sokoni mwaka 2021. 

EP ya Wave imesheheni ngoma 6 na Kati ya hizo Joh Makini ameshirikiana na wasanii wa tatu ambao ni G Nako, Ottuck William pamoja na Damian Soul ambaye amemshirikisha kwenye ngoma ya “Too Much”. 

Akizungumza kwenye Amplifaya ya Clouds FM  hivi karibuni, Joh Makini alidokeza kidogo kuhusu EP hiyo ambapo Ali sema kuwa hii ni EP yake ya kwanza kwenye muziki na kwamba hyenas akaongeza kwa kuitazama albamu siku za mbeleni 

"Hii ni EP yangu ya kwanza kwenye rekodi zangu, nadhani mwaka huu itakua tofauti kidogo usishangae kukawa labda na EP mbili na kisha album kabla mwaka haujaisha" 

Leave your comment