Ngoma Zinazotamba Tanzania Wiki Hii

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwandishi: Charles Maganga

Tasnia ya muziki nchini Tanzania imeendelea kufanya vizuri haswa ukizingatia kwamba mashabiki wameendelea kupokea burudani kali kutoka kwa wasanii ambao wameachia ngoma zenye ladha tofauti kama Amapiano, Bongo Hip Hop, Singeli na Bongo Fleva 

Kuanzia kwa JohvMakini mpaka kwa Rayvanny ambaye amekosha mashabiki kwa kuachia kibao chake kipya, hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania wiki hii : 

Mind Your Business - Darassa 

Darassa aanaendelea kukumbusha mashabiki zake kuwa amerudi kwenye muziki na hii ngoma yake mpya ya kuitwa “Mind Your Business” bila shaka imekosha wengi sana. Hii ni ngoma yake ya 3 kwa mwaka huu baada ya “Dead Zone” na “Nobody” aliyomshirikisha Bien 

Wave EP - Joh Makini

Joh Makini ameachia EP yake iliyosubiriwa kwa hamu sana ya kuitwa Wave ambayo ina ngoma 6 za moto na kati ya hizo amewashirkisha wasanii ambao Ottuck William, Damian Soul na G Nako. Hii Ni EP ya kwanza kutoka kwa Joh Makini tangu aanze muziki.

One Day Yes - Rayvanny 

Mserereko wa burudani kutoka kwa Rayvanny umezidi kuwa mkali kwani wiki hii fundi huyu wa Bongo Fleva aliachia “One Day Yes” ngoma bsyo ndani yake anaelezea kwa undani maumivu ya mapenzi anayopitia baada ya kupigwa kibuti na binti ampendaye.

Namficha - DJ Joozey Ft Harmonize 

Kwenyr ngoma hii ya “Namficha” sio tu kwamba utapenda beat zuri la DJ Joozey lakini pia utapenda ujumbe wa Harmonize ambao umejaa mafunzo na kuakisi maisha ya kila siku.

Nani - Abigail Chams Ft Marioo 

Kupitia wimbo huu Marioo anamkaribisha rasmi Abigail Chams kwenye uwanja wa Amapiano ambapo wawili hawa wanatumia sauti zao kueleza kwa namna gani wanapendana kwa dhati.

Leave your comment