Nyimbo Mpya Tanzania:P Funk Majani Awaunganisha Rapcha Na Conboi Kwenye Ngoma Mpya “Tunashine”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ni ukweli ulio wazi kwamba P Funk Majani ni moja kati ya watayarishaji bora sana wa muziki Tanzania na hivi karibuni ameamua kuthibitisha hilo kwa kuachia ngoma mpya “Tunashine” ambayo amewashirikisha Rapcha na Conboi

Ujio huu mpya wa P Funk Majani ulikuwa unasubiriwa na wengi sana hasa wapenzi wa muziki wa Hip Hop kwani kwa muda mrefu sasa amekuwa akidokeza ujio wa ngoma hii.

Kwenye mkwaju huu wa Hip Hop, Rapcha na Conboi wanasimulia na kuzungumzia kuhusu harakati za kwenye maisha, changamoto walizopitia na namna ambavyo wanataka waende mbali kwenye maisha ili waweze ku-shine.

Ngoma hii imesindikizwa na video kali ambayo imeongozwa na Director Black X ambaye ameshafanya video tofauti tofauti ikiwemo “Watu” Ya Belle 9, “Wanijue” Ya Micky Singer pamoja na “Pombe Na Muziki” Ya Kwake Mr Blue na Steve RnB.

https://www.youtube.com/watch?v=ah-VkUea6VU

Leave your comment