Hatimaye Navy Kenzo Waachia Album Ya "Most People Want This"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kundi la Navy Kenzo kutoka nchini Tanzania, hatimaye wameachia albamu yao ambayo ilikuwa inasubiriwa sana na mashabiki ya kuitwa "Most People Want This"

Kwa mara ya kwanza Navy Kenzo walitangaza ujio wa albamu hiyo mwanzoni mwa mwezi Februari na hii ni albamu ya tatu kutoka kwa Navy Kenzo. Albamu nyingine kutoka kwa kundi hilo ni pamoja na "Above In A Minute" pamoja na "Story Of The African Mob"

Albamu ya "Most People Want This" imesheheni ngoma 12 na kati ya hizo, ngoma tatu ambazo ni "Manzese", "Hold On" Featuring Fireboy DML pamoja na "Don't Let Go" zilikuwa zimeshatoka huku msanii pekee ambaye ameshirikishwa kwenye albamu hiyo ni Fireboy DML kutoka nchini Nigeria.

Kutoka kwenye ngoma mbalimbali ya albamu hii, Navy Kenzo wamegusia mambo tofauti tofauti kwenye albamu hii ikiwemo Raha ya kuwa na mpenzi, kuvumiliana huku baadhi ya ngoma zikiwa zimelenga hasa kukosha watu wanaopenda starehe na kwenda club.

https://www.youtube.com/watch?v=rz1RhbRmcrY

Leave your comment