Nyimbo Mpya Tanzania Wiki Hii: Zuchu 'Napambana', Ibraah 'Nimepona'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Mwezi Machi umeanza kwa kasi sana kwani wasanii tofauti tofauti kutoka Tanzania wameendelea kuporomosha burudani kali kwa mashabiki zao kwa lengo la kuwaburudisha, kuwafurahisha na kuwaelimisha pia.

Kutoka kwa wasanii kama Zuchu, Ibraah, Kayumba na wengineo wengi hizi hapa ni ngoma mpya kutoka Tanzania kwa wiki hii :

Napambana - Zuchu

Baada ya kukutana na changamoto mbalimbali, Zuchu aliamua kuandika ngoma yake ya Napambana ambayo ndani yake anaapa kupambana na kuvuka vikwazo vingi ambavyo anakutana navyo. Aidha, Zuchu pia amesindikiza ngoma hii na video kali ambayo imeongozwa na Director Folex

https://www.youtube.com/watch?v=WpvN2fDsqsg

Fine Tape - Kayumba

Baada ya kuidokeza kwa muda mrefu, hatimaye wiki hii, Kayumba aliachia albamu yake ya kuitwa Fine Tape yenye ngoma 12 ambayo ndani yake ameshirikisha wasanii tofauti tofauti kama Rayvanny, Roma, Maudi Elka na Harry Song. Hii ni albamu ya kwanza kutoka kwa Kayumba

https://www.youtube.com/watch?v=xEmEwt8aqLE

Nimepona - Ibraah

Kama ulikuwa ume-miss muziki mzuri kutoka kwa Ibraah basi amekuletea hii hapa ya kuitwa Nimepona. Kwenye ngoma hii, Ibraah anaweka wazi maumivu aliyopitia baada kuachwa na kupitia mkwaju huu, Ibraah anadokeza zaidi kuwa maumivu yake yalishapona.

https://www.youtube.com/watch?v=kbBqFh0UTrg

Rara - Phina Featuring Jux

Phina ameuanza vyema mwaka 2023, na ngoma yake hii ya kuitwa Rara ambayo amefanya na Jux. Kwenye ngoma hii utafurahia mashahiri mazuri kutoka kwa Phina pamoja na beat zuri ambalo limepamba vyema ngoma hii

https://www.youtube.com/watch?v=KZrB2qWDtVg

Adela - Ben Pol

Baada ya “Wewe”, Adela ameachia ngoma hii ya kuitwa Adela, ngoma ambayo ndani yake Ben Pol anaugulia maumivu ya mapenzi.

https://www.youtube.com/watch?v=jI40d_f7C2w

Leave your comment