Zuchu Aachia Video Mpya 'Napambana'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii nguli kutoka Tanzania, Zuchu hatimaye ameachia video ya wimbo wake ambao kwa sasa unatamba nchini Tanzania na Africa Mashariki wa kuitwa Napambana.

Ngoma ya Napambana iliachiwa Machi 3,  2023 ikiwa ni ngoma ya pili kutoka kwa Zuchu kwa mwaka huu wa 2023 baada ya kuachia Utaniua ngoma ambayo ilipokelewa vyema sana na mashabiki.

Video ya Napambana imepambwa na stori nzuri ambayo inamuonesha Zuchu akivaa uhusika wa binti anayeishi kijijini akiwa ni kibarua kwenye shamba la chai na kisha baadae anaamua kuhamia mjini ambapo anakutana na changamoto mbalimbali pamoja na kudharauliwa na mabinti wenzake.

Video ya Napambana imeongozwa na Director Folex ambaye ameshiriki kuandaa video mbalimbali ikiwemo Siwezi ya Feza Kessy pamoja na Puuh Lyrics video ya kwake Billnass akiwa na Jay Melody. 

https://www.youtube.com/watch?v=WpvN2fDsqsg

Leave your comment