Exclusive DJ Mixes and 100% Ad-Free Music!
Micky Singer Aachia Ngoma Mpya “Jishaue” Akiwa Na Tommy Flavour
6 March 2023

[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Kama ulikuwa na mawazo au huzuni, shaka ondoa kwani msanii kutoka nchini Tanzania, Micky Singer ameachia mkwaju mpya kabisa wa kuitwa Jishaue wenye lengo la kukuchangamsha na kukuburudisha.
Baada ya kuwapa mashabiki zake “Nobody” takriban wiki mbili zilizopita, Micky Singer amerudi na Jishaue, ngoma ambayo amemshirikisha msanii kutoka Kings Music Tommy Flavour.
Micky alidokeza ujio wa collabo hii na Tommy Flavour mwishoni mwa mwaka jana kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kwenye Jishaue, Micky kaja kitofauti ambapo kwani kwenye ngoma hii anasisitiza, watu wafurahi, wajikubali na kujipigia makofi kutokana na mambo mazuri ambayo wamefanya. Kama kawaida ya Micky Singer, Jishaue pia imeundwa na mashahiri yaliyojaa ucheshi na mistari ya kumfanya mtu afurahi.
Weekly Top 10 songs
Top stories
- The Marathon
25 April
- MOSS Kay
24 April
- Cashout by monyzoh boy
24 April
- Naphlic_fx
24 April




Leave your comment