Ibraah Aachia Ngoma Mpya “Nimepona”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Fundi wa muziki huu wa Bongo Fleva, Ibraah ameendelea kuupamba vyema mwaka 2023 na hii ni baada ya kuachia kibao chake kipya cha kuitwa Nimepona.

Ibraah amesainiwa kwenye lebo ya Konde Music Worldwide, ambayo inamilikiwa na Harmonize na ngoma yake hii ni ya pili kwa mwaka 2023 baada ya Tunapendeza ambayo alifanya na Harmonize.

Kwenye Nimepona Ibraah, anaugulia maumivu ya mapenzi ambapo mwanzo mwisho anasimulia namna ambavyo alikuwa anampenda mwenza wake kwa dhati ila baada ya muda mpenzi wake huyo akamkimbia na kupitia kibao hiki, Ibraah anaonesha kukubali matokeo na anaapa kuendelea na maisha.

Ngoma hii kutoka kwa Ibraah inatukumbusha ngoma zake za zamani kama Nitachelewa, Wa Ndoto, Sitosema na nyinginezo nyingi ambazo alizitendea haki.

https://www.youtube.com/watch?v=kbBqFh0UTrg

Leave your comment