Zuchu Akosha Mashabiki Na Ngoma Mpya “Napambana”

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Msanii nguli kutokea nchini Tanzania, Zuchu hivi karibuni ameachia mkwaju wake mpya kabisa wa kuitwa Napambana ambao umepokelewa kwa mikono na miwili na mashabiki. 

Napambana ni ngoma ya pili kutoka kwa Zuchu kwa mwaka huu wa 2023 na inakuja takriban wiki mbili tangu aachie ngoma yake ya Utaniua ambayo aliitoa kwa mashabiki zake kwa ajili ya  kipindi cha Valentine.

Kwa mujibu wa Zuchu, Napambana ni ngoma yenye lengo la kutia watu moyo na kuwapa faraja pale ambapo wanakutana na changamoto mbalimbali kwenye maisha. Zuchu alidokeza pia kwamba aliandika ngoma hii katika kipindi ambacho alikuwa na changamoto ya kifedha wakati akiwa kwenye muziki.

Kwenye Napambana, Zuchu anatumia lugha ya stara ana Kiswahili sanifu ili kupamba ngoma hii ambayo imetayarishwa na Mocco Genius, mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania. 

https://www.youtube.com/watch?v=lxIn9z_hnRc

Leave your comment