Darassa Aachia Ngoma Mpya “Nobody” Akiwa Na Bien

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Itoshe kusema kwamba Mr Burudani, Darassa CMG amerudi rasmi kwenye kiwanda cha muziki Tanzania na hii ni kupitia mkwaju wake mpya kabisa wa kuitwa Nobody ambao amefanya na Bien kutokea huko nchini Kenya.

Rekodi zinasema kuwa, kwa mwaka 2022 Darassa alikuwa kimya bila kutoa ngoma yoyote na kabla ya ngoma hii, Darassa siku chache zilizopita aliachia Dead Zone, hivyo kufanya Nobody kuwa ngoma yake ya pili kwa mwaka huu wa 2023

Ndani ya Nobody, Darassa anaimbia mapenzi ambapo kupitia kibao hiki Mr Burudani anamuhakikishia mwandani kwamba yuko nae pamoja na hakuna mtu yeyote ambaye anaweza kuwatenganisha wawili hao.

Bien ambaye ni mshiriki wa kundi la Sauti Sol amepamba ngoma hii na sauti yake mujarab hasa kwenye sehemu ya kiitikio ambapo Bien ameweza kupatendea haki vilivyo.

Nobody imetayarishwa na Abbah Process, mtayarishaji wa muziki kutoka Tanzania ambaye ametayarisha ngoma nyingi ikiwemo hii inayotamba kwa sasa Nakuja ya kwake Tommy Flavour akiwa na Marioo.

https://www.youtube.com/watch?v=t1EBvgjw2Ac

Leave your comment

Top stories

More News