Stamina Aachia Ngoma Mpya Machozi Ft Bushoke

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Rapa mwenye heshima yake kwenye muziki wa Tanzania Stamina Shorwebwenzi amerudi kivingine na ngoma yake mpya ya kuitwa Machozi akiwa amemshirikisha Bushoke.

Kama kuna kitu ambacho mashabiki wanafahamu kuhusu Stamina basi ni uwezo wake wa kuandika ngoma zenye ujumbe zilizonakshiwa na hadithi nzuri na baadhi ya ngoma hizo ni pamoja na Ukizaliwa, Future Wife na Baba.

Kwenye Machozi Stamina analalamika kuhusu mkewe ambaye sio mwaminifu kwenye mahusiano. Humu ndani utasikia kwa upana na marefu malalamiko yake kuhusu namna ambavyo mkewe anachepuka nje ya ndoa na namna ambavyo Stamina kama mume, alikuwa anajitahidi kutunza familia yake.

Hii ni ngoma ya kwanza kwa Stamina kwa mwaka huu na imetayarishwa na Sampamba kutoka Tanzania.

https://www.youtube.com/watch?v=djABvQoYiPQ

Leave your comment