Rapa Darassa Arudi Kivingine Na Ngoma Mpya 'Dead Zone' 

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye rapa Darassa ameamua kwa mara nyingine kunogesha kiwanda cha muziki Tanzania kwa kuachia mkwaju mpya kabisa wa kuitwa Dead zone

Rapa huyo ambaye aliiteka Tanzania mwaka 2016 na ngoma yake ya muziki ameachia ngoma hiyo ya Deadzone ikiwa ni ngoma yake ya kwanza kutoka kwake kwa mwaka 2022 na mwaka 2023 Kwani mara yake ya mwisho kuachia ngoma ilikuwa ni Desemba 2021 alipoachia Sogea akiwa na Sani Boy

Kwenye Dead zone, Darassa anatoa nasaha kuhusu maisha ambapo anazungumzia jinsi ambavyo hana uoga na maisha huku akiwapa onyo maadui na watu wanaofuatilia maisha yake. Ngoma hii imetayarishwa na Mr T Touch ambaye pia alihusika kutayarisha ngoma ya Mziki

Dead Zone pia imesindikizwa na video kali yenye stori nzuri na ambayo inaendana mashahiri ya ngoma hii, video ambayo imetayarishwa na Hanscana.

https://www.youtube.com/watch?v=R8ln5pIkp04

Leave your comment