Wasanii 6 Chipukizi wa Kushabikiwa Kutoka Afrika Magharibi

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Muziki wa Afrika Magharibi imekuwa ni biashara kubwa sana na hii ni kutokana na kuwepo kwa wasanii wengi wazuri ambao wanajua kukidhi haja za mashabiki pamoja na kutambulika kwa muziki wa Afrobeats ambao imezidi kukua kila siku.

Afrobeats imeanzia huko nchini Nigeria na kufikia sasa aina hiyo ya muziki imeleta aina nyingine tofauti tofauti za muziki kitu kilichopelekea ukuaji wa muziki wa Afrika Magharibi.

Uwepo wa aina tofauti tofauti za muziki kama vile highlife, Hip life, Asakaa, pop na drill umechagiza mno ukuaji wa muziki, ukijumlisha na uwekezaji mkubwa unaofanyika bila shaka wasanii wengi wamehamasika kutengeneza muziki wenye hadhi ya kimataifa.

Mdundo inakuletea orodha ya wasanii kutokea Afrika Magharibi ambao wanakuja kwa kasi sana :

Tar1q

Tar1q (Tah-reek) ni mwimbaji na mwandishi kutokea Nigeria ambaye amesainiwa  na Nutrybe, shule ya muziki ambayo iko chini ya lebo ya Chocolate City na ni katika shule ambapo Tar1q ameweza kujinoa zaidi kwenye suala zima la uandishi.

Mwanamuziki huyu amebarikiwa na sauti Tamu pamoja na utumbuizaji mkali akiwa jukwaani na muda si mrefu anaenda kuwa mfalme wa Afro rhythm, ambayo ni mtindo mpya kabisa wa muziki.

Afro Rythm inaunganisha Afrobeats mambo leo, Pop, Hiphop na R&B na yeye kuimba aina hii ya muziki imefanya awe maarufu sana. Baadhi ya ngoma zake ni pamoja na Bad Intentions, Signal na Emotions.

Wasanii wanaomkosha zaidi ni pamoja na Wizkid, J Cole, Kwam 1 na Chris Brown.

Young Jonn

Bila shaka kama umesikiliza ngoma kama Xtracool, Dada Remix, Normally, If You Leave na nyinginezo nyingi basi bila shaka utakuwa unamfahamu Young John.

Nyota huyu kutokea Ibadan alianza kama mtayarishaji wa muziki wa Afropop na baadae akahamia kuwa msanii mwenye mafanikio . Kipaji na uhodari wake kwenye muziki imetumika kutengeneza ngoma kama Mafo ya Naira Marley pamoja, Story For The God's Ya Olamide Baddo na ya hivi karibuni Don't Call Me ya kwake Lil Kesh.

Blaqbonez

Rapa huyu wa Nigeria ni kipaji kingine kutokea lebo ya Chocolate City. Mapenzi yake na muziki yalianza kipindi akiwa na miaka 13 na alikuwa ni hodaei sana kwenye ku-rap japo wazazi wake hawakupendezwa na chaguo lake la kuwa rapa.

Alipoingia kwenye Chuo Cha Obafemi Awolowo ndipo mapenzi yake na muziki wa rapa yalikua zaidi ambapo alikuwa anashiriki kweye mashindano ya ku-rap na ndipo hapo akaanza kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kuitangaza zaidi mpaka kuwa maarufu.

Blaqbonez kwa sasa ni moja kati ya Marapa bora wenye ngoma kali kama Fashion, Back In Uni, Commander, Whistle na Go Home.

Candy Bleakz

Candy Bleakz anavaa kofia nyingi sana kwani yeye ni rapa, mwandishi wa ngoma pamoja na mwigizaji na kwa dhati kabisa amekuwa akitendea haki nafasi zote hizo. Mashahiri yake mazuri yamempa jina la "The Queen Of Streets" na ni jina ambalo anajivunia kuwa nalo.

Uandishi wake mujarab ulianza tangu akiwa sekondari lakini mambo yote yalibadilika baada ya kushinda shindano la Lagos Got Talent ambalo lilimkutanisha na MI Abaga ambaye kwa kipindi hicho alikuwa ni CEO wa Chocolate City.

Kwa sasa Ukisikia Ngoma kama Tikuku, Red, Dragon Anthem na Kelegbe unatamba kabisa ni kwa namna gani Candy Bleakz ana ushawishi wenye nguvu kwenye soko la rap la Afrika Mashariki.

Major AJ

Major AJ ni rapa na mwanamuziki wa Afro fusion ambaye amezaliwa eneo la Kkpokwu huko Benue. Baada ya kushiriki kwenye kwa ya ya kanisani alipokuwa kwao na kuanza kusikiliza muziki wa Hip Hop na Afrobeats, nyota huyu akajenga mapenzi makubwa ya muziki japo hakuanza muziki rasmi mpaka 2019.

Akiwa mwanafunzi kwenye Chuo Cha Ilorin Major AJ alijikita kwenye eneo la  Computer Science na alitengeneza mapenzi na muziki wa Hiphop baada ya kusikiliza wasanii kama Lil Wayne, Ice Prince, Choc Boys na wengineo wengi na ndipo hapo alianza kurap na kutengeneza ngoma kama Ominirascal, Taboo na Superstar.

Noon Dave

Noon Dave ni kipaji kingine kutoka Chocolate City na amekulia mjini Lagos sehemu ambayo  amekutana na mengi mazuri kuhusu muziki. Wakati akiwa ni kijana barubaru kabisa alikuwa akisikiliza mitindo mbalimbali ya muziki kitu ambacho kimefanya yeye kuwa na utajiri wa mwingi wa aina za muziki  

Wasanii kama J Cole, Burna Boy, Drake, Eminem, Kendrick Lamar, Bryson Tiller na Party next door wamechagiza yeye kufanya muziki mpaka kuachia ngoma yake kali ya Brunch.

Leave your comment