Tommy Flavour Adokeza Ujio Wa Nakuja Remix Akiwa Na Ali Kiba

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kwa sasa nchini Tanzania, ngoma inayosumbua zaidi kwenye mitaa na vyombo vya habari ni Nakuja ya kwake Tommy Flavour akiwa amemshirikisha Marioo na hivi karibuni msanii huyo amedokeza ujio wa remix ya wimbo huo.

Nakuja ni ngoma ambayo imeachiwa hivi karibuni na Tommy Flavour ambapo msanii huyo alidokeza hivi karibuni kuwa wazo la kumshirikisha Marioo lilitoka kwenye uongozi wa Kings Music  ambao walishauri msanii huyo amshirikishe Marioo. Kwenye mtandao wa Youtube, Nakuja imeshajikusanyia watazamaji takriban laki 3 ndani ya siku 6 tu.

Wakati ngoma hiyo ikiendelea kufanya vizuri, hivi karibuni Tommy Flavour amedokeza kupitia ukurasa wake wa Instagram kuwa huenda akaachia remix ya ngoma hiyo akiwa amemshirikisha bosi wa lebo ya Kings Music, Ali Kiba.

Tommy Flavour alichapisha video ya Ali Kiba akiwa anaimba ngoma ya Nakuja na kuandika "Eti wangapi mko tayari kuona remix ya Nakuja na King Kiba"

Ikumbukwe kuwa Tommy Flavour na Ali Kiba walishawahi kukutana kwenye ngoma kadhaa ikiwemo Umukwano, Jah Jah, Ndombolo pamoja na Tamba ambayo inapatikana kwenye albamu ya Ali Kiba ya kuitwa Only One King.

https://www.youtube.com/watch?v=UviYi2oqHos

Leave your comment

Top stories

More News