Wasanii 5 Kutoka Tanzania Ambao Wameshawahi Kutoa Ngoma Za 'Valentine'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Ni ukweli kwamba kuna watu njia nyingi sana ambazo watu wanaweza wakasherehekea Valentine na mojawapo ya njia hizo ni kupitia muziki unaoenda sawia na msimu huo wa Valentine.

Ili kuweza kuburudisha watu katika msimu huu wa wapendanao baadhi ya wasanii kutoka Tanzania kwa nyakati tofauti tofauti wameachia ngoma kwa ajili ya msimu huo wa Valentine. Wafuatao ni wasanii watano kutoka Tanzania ambao wana ngoma maalum kwa ajili ya msimu wa Valentine

Kusah

Februari 14 mwaka 2021, Kusah alichachua siku ya Valentine kwa kuachia "My Valentine" ngoma ambayo ndani yake anamwaga sifa za kutosha kwa mpenzi wake huku akionesha ni kwa namna gani amezama kwenye penzi la mwenza wake huyo.

https://www.youtube.com/watch?v=futRUATLXTc

Rayvanny

Ndani ya dakika 1 na sekunde 24 Rayvanny kupitia ngoma ya hii ya kuitwa "Valentine" aliweza kusema yote ya moyoni mwake kuhusu mapenzi. Kwenye ngoma hii utapenda namna ambavyo Rayvanny anatoa sifa na tabia za mpenzi wake kwa ukamilifu na bila shaka hii ni moja kati ya ngoma bora za Valentine kutoka Tanzania

https://www.youtube.com/watch?v=TWbPaDHonrc

B2K

Mwaka 2022 B2K alinogesha shamrashamra za sikukuu ya wapendanao na ngoma yake ya Valentine na ujumbe mzima wa kwenye ngoma hiyo ni mmoja tu kwamba, maneno ya watu pamoja na husda zao kamwe haziwezi kuvunja penzi alilonalo kwa mwandani wake.

https://www.youtube.com/watch?v=GF51eDe4CuA

Beka Flavour

Kama una mpenzi na unataka kumuonesha ni kwa namna gani unampenda na kumjali basi namna nzuri ya kueleza hisia zako ni kupitia ngoma hii ya kuitwa Valentine ya kwake Beka Flavour, ngoma ambayo ina mashahiri mazuri ya mapenzi pamoja na melody kali mahususi kabisa kwa ajili yako

https://www.youtube.com/watch?v=yxWK7rI_R40

Mac Voice

Kabla ya kujiunga Next Level Music, Mac Voice ambaye kipindi hicho alikuwa anatumia jina la Maka Voice alikosha wapendanao wengi na ngoma yake ya kuitwa Valentine. Kwenye "Valentine" Mac Voice anamtakia mpenzi wake heri ya Valentine na kumtaka aongeze mapenzi zaidi.

https://www.youtube.com/watch?v=3YcN8bTfWXA

Leave your comment