Navy Kenzo Watangaza Ujio Wa Albamu Yao Mpya

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kundi la muziki kutoka Tanzania, Navy Kenzo wameendelea kuporomosha burudani kwa mashabiki zao baada ya hivi karibuni kutangaza kuwa ifikapo mwezi Machi huu wataachia albamu yao mpya.

Navy Kenzo ambalo ni kundi lililoundwa na Aika pamoja na Nahreel ambaye pia ni mtayarishaji wa muziki wametoa taarifa hiyo ikiwa imetimia takriban miezi 7 tangu waachie Manzese na miezi 2 tangu waachie Hold On wakiwa wamemshirikisha Fireboy DML

Kwenye ukurasa wake wa Instagram, Navy Kenzo wametangaza kwamba albamu yao itaitwa Most People Want This na inatarajiwa kuingia sokoni Tarehe 9 mwezi Machi. Navy Kenzo waliongeza kwa kudokeza kuwa ngoma ya kwanza kutoka kwenye albamu hiyo itatoka leo usiku wa manane.

Ikumbukwe kwamba hii inatarajiwa kuwa ni albamu ya tatu kutoka kwa Navy Kenzo tangu aanze muziki. Albamu yao ya kwanza iliyoitwa Above In A Minute ilitoka mwaka 2017 ikifuatiwa na Story Of The African Mob ya mwaka 2020.

Leave your comment