Uhakiki Wa Vichwa Vya Habari Vya Magazeti ya Tanzania Leo 07-02-2023.

[Picha:Millard Ayo]

Mwandishi: Stellah Julius

Pakua na Kusoma matukio ya Magezitini ndani ya Mdundo

Jamii ya wapemba wanaoishi Kenya hatimaye wamepatiwa uraia wa nchi hiyo waliokuwa wakiusubiri kwa muda. Rais wa nchi hiyo William Ruto alitangaza kupatiwa kwa uraia Wakenya hao walikuwa wakiishi maeneo ya Mombasa, Lamu, Kilifu na kwale. Kuhama kwa wapemba kutokea Tanzania kulitajwa kuwa ni sababu za machafuko yaliyotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 nchini Tanzania. (Jamhuri)

Digrii za mchongo zazua mzozo mara baada ya mbunge wa Morogoro vijijini Hamis Taletale kutunukiwa shahada ya Uzamivu na taasisi ya isiyo ya kiserikali ya Academy of Universal Global Peace ya nchini Marekani. Baada ya tukio hilo mjadala umezuka ukidai taasisi isiyo ya kiserikali siyo jukumu lake kutoa shahada hizo bali hutolewa na taasisi za elimu zinazoeleweka kama chuo kikuu Cha Dar es salaam. (Jamhuri)


Baada ya ajali kutokea mkoani Tanga na kuuwa watu 20, wachawi wa ajali hiyo wametajwa ikiwemo rushwa wanazozipokea askari wa barabarani, mbali na rushwa pia ubovu wa miundombinu, pamoja na madereva wasio na sifa ya kuendesha vyombo vya moto. Hayo yalibainishwa Bungeni wakati mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya Bunge ya mambo ya nje ulinzi na usalama Vita Kawawa alipokuwa akiwasilisha ripoti ya utekelezaji wa kipindi cha Februari 2022 hadi Januari 2023. (Mwananchi)

Mama mzazi wa Erick Kwai, Leornida Mosha amethibitisha kutokumzika mwanae huyo mara baada ya kutekeleza mauaji ya dada yake wa kufikia Anna Thomas yaliyotokea siku ya Jumamosi. Baada ya mauaji hayo mama huyo amesema hatomsafirisha mwanae kwenda mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya maziko na pia tayari ameshateketeza vitu vya kijana wake Erick kwa moto. (Mwananchi)

Jeshi la kujenga Taifa (JKT) limeng'aka vikali mara baada ya vyombo vya habari kutoa ripoti ya vijana 147 wa jeshi hilo kuwa na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kusema huo ni udhalilishaji kwa JKT. Hayo aliyasema Mkuu wa tawi la utawala Brigedia generali Hassan Mabena wakati alipokuwa akiongea na vyombo vya habari jijini Dodoma huku wakivitaka vyombo hivyo kufuta picha walizoziambatanisha na taarifa hiyo pamoja na kuomba radhi. ( Majira)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema anajivunia mafanikio ya Chama Cha Mapinduzi wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama hicho yaliyofanyika visiwani Zanzibar. Rais Mwinyi akielezea utekelezaji wa Ilani ya Chama ya Mapinduzi kama muongozo wa mafanikio hayo ambayo ni pamoja na Ujenzi wa uchumi wa bluu pamoja na maridhiano ya kisiasa yaliyofanyika dhidi ya wapinzani. (Uhuru)

 

Leave your comment