Uhakiki Wa Vichwa Vya Habari Vya Magazeti ya Tanzania Leo 06-02-2023

[Picha:Millard Ayo]

Mwandishi: Stellah Julius

Pakua na Kusoma matukio ya Magezitini ndani ya Mdundo
Hospitali ya Rufaa ya Bugando imeanza uchunguzi katika samaki wanaopatikana katika mikoa ya kanda ya ziwa. Agizo Hilo lilitokewa na Makamu wa Rais Dk Philip Mpango baada ya kusadikika kuwa samaki wanaopatikana maeneo hayo huhifadhiwa kwa maji ya maiti na kupelekea ongezeko la magonjwa ya saratani katika ukanda huo. Mkuu wa idara ya saratani hospitali ya Bugando Dk. Nestory Masalu alisema hospitali hiyo tayari imekusanya sampuli 7000 za wagonjwa wenye saratani na nyingine 7000 za wagonjwa wasio na saratani na taratibu za uchunguzi huo alisema utachukua takribani miezi sita kutokana na ukubwa wa tatizo hilo. ( Nipashe)

Kijana wa miaka 32 Erick Kwai ameuwawa na wananchi wenye hasira Kali mara baada ya kumuua dada yake wa kufikia pamoja na kumchoma mama yake kisu. Katika tukio hilo Mwenyekiti wa eneo hilo alisema ya kuwa kijana huyo alikuwa na magonjwa ya akili kutokana na uvutaji wa bangi uliopelekea afikishe hospitali mwaka jana mwezi Machi. Pia kamanda wa polisi mkoa wa Dar es salaam Jumanne Murilo alisema polisi walipata taarifa za tukio hilo lakini tayari mtuhumiwa alikuwa ameshauwawa na wananchi wenye hasira Kali (Nipashe)


Siri nzito zabainishwa katika ajali iliyowauwa ndugu walipokuwa wakisafirisha msiba iliyotokea mkoani Tanga katika wilaya ya Korogwe. Katika ajali hiyo watumishi wa afya katika hospitali ya Magunga walisimamishwa kazi baada ya kuchelewa kufuka katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya kutoa huduma na kupelekea kugharimu maisha ya watu. Serikali imejitolea kugharamikia misiba yote 21 huku ikitoa Shilingi milioni 3 kwa ajili ya chakula. Aidha Omar Mgumba ambaye ni Mkuu wa mkoa wa Tanga alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa Lori ambalo lilikuwa likijaribu kulipita gari la mbele yake bila ya tahadhari. (Majira)

Taasisi ya Benjamin Mkapa imezindia programu ya Mama na mwana mkoani Songwe ambayo itasaidia wajawazito pamoja na wale wenye watoto chini ya mwaka mmoja kutoa mrejesho juu ya huduma wanazopatiwa katika vitu vya afya kupitia simu. Program hiyo ilizinduliwa na Clarence Mkoba ambaye ni mratibu wa program hiyo katika kituo cha Mbeya. Pia Rebecca Ndawala ambaye ni mratibu wa huduma ya afya ngazi ya jamii Mbozi alisema program hiyo itasaidia kupunguza urasimu kutokana na upatikanaji wa majibu ya maswali kutoka kwa wananchi kwa haraka. (Majira)

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mjumbe wa kamati ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Dk Philip Mpango amewataka viongozi wa CCM kufanya siasa za kujenga Taifa. Dk. Mpango aliyasema hayo wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama hicho yaliyofanyika jijini Dar es salaam na pia aliwataka viongozi wa chama hicho kushirikiana na serikali katika kuwahimiza wananchi kulipa Kodi kwa maendeleo ya Taifa. Katika maadhimio hayo wanachama wapya 580 walijiunga na Chama hicho. (Zanzibar Leo)

Makamu wa pili wa Rais Zanzibar na mlezi wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Tanga Hemed Suleiman Abdallah amempongeza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kutokana na maendeleo katika sekta ya miundombinu. Hayo aliyasema wakati alipokuwa akikagua miradi mbalimbali wilayani pangani na kuwataka wakandarasi kutumia fedha za miradi kwa nidhamu. (Zanzibar Leo)

Mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia kutokana na utekelezaji wake wa Ilani za Chama hicho kwa vitendo. Hayo aliyasema Majaliwa wakati wa maadhimisho ya miaka 46 ya Chama Cha Mapinduzi yaliyofanyika kitaifa mkoani Kigoma wilayani kasulu na kusema ya kuwa Chama Cha Mapinduzi Kiko imara na kitaendelea kutekeleza Ilani za wananchi. (Tanzania Leo)

Leave your comment