G Nako Aachia Ep Yake Ya 'Make You Dance'

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Fundi wa muziki wa Hiphop kutoka Tanzania G Nako hatimaye ametimiza ahadi aliyoiweka kwa muda mrefu baada ya hivi karibuni kuachia EP yake ya "Make You Dance"

G Nako ambaye ni moja ya mshiriki kwenye kundi la Weusi ameachia EP hiyo baada ya kuidokeza kwa muda mrefu sana. Make You Dance ni EP ya kwanza kutoka kwa G Nako na kwa mujibu wa G Nako, EP ya "Make You Dance" ina lengo la kusherehesha na kufanya watu wacheze pindi wawapo sehemu za starehe.

Make You Dance EP imesheheni ngoma 7 ambazo ndani yake G Nako ameshirikisha wasanii tofauti tofauti kama Femi One kutokea nchini Kenya, Dreygon, Tasiana, Young Dar Es Salama pamoja na Rayvanny ambaye ameshirikishwa kwenye ngoma ya "Tusipangiane"

Ngoma nyingi kwenye EP hii ya "Make You Dance" zimetengenezwa kwa namna ambayo inalenga kuamsha vibe na mizuka ya msikilizaji na pamoja na kwamba G Nako anasimama na kutambulika kama moja ya waandishi bora Tanzania lakini kwenye EP hii, G Nako amelenga zaidi kuburudisha kuliko kuonesha ufundi wake kimashahiri.

Leave your comment