Q Chief Aachia Tracklist Ya Album Yake "The Last Meal"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye nguli kutokea Bongo Flevani, Q Chief, ameamua kurudi tena kwenye muziki baada ya hivi karibuni kuachia tracklist ya albamu yake ya kuitwa The Last Meal ambayo inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.

Q Chief ni msanii kutokea Tanzania ambaye alianza muziki akiwa na miaka 18 na kujiunga na kundi la muziki linaloitwa Mzimuni Family na ni hapo alipo pata nafasi ya kurekodi chini ya Jimmy Master. Baadhi ya ngoma zake zilizompatia umaarufu mkubwa ni pamoja na "Tutaonana Wabaya" "U Hali Gani" "Kama Yule" na nyinginezo nyingi.

The Last Meal ni albamu ya kwanza ya Q Chief ndani ya miaka kumi na bila shaka mashabiki wengi wamekuwa na hamu ya kumsikia Q Chief mpya.

[Picha: Instagram]

Kupitia ukurasa wake wa Instagram hivi karibuni Q Chief  ameachia orodha ya nyimbo zilizokuwemo kwenye albamu yake hiyo mpya. Albamu ya The Last Meal imesheheni ngoma 10 na ndani yake ameshirikisha wasanii watano kama Dogo Janja, Bushoke, Professor Jay, Tamimu pamoja na Kusah ambaye ameshirikishwa kwenye ngoma namba 7 ya kuitwa Tiktok.

Kando na Q Chief, wasanii wengine wanaotarajia kuachia kuachia miradi yao ya muziki hivi karibuni ni pamoja na Linex ambaye anatarajia kuachia EP yake, Rayvanny anayetarajia kuachia Flowers III pamoja na Maua Sama anatarajia kuachia albamu yake ya Love Waves.

Leave your comment