Nyimbo Mpya: Tommy Flavour & Marioo - Nakuja

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Katika harakati za kuitangaza Bongo Fleva na kuburudisha mashabiki, mafahali hawa wawili yaani Tommy Flavour pamoja na Marioo wametoa diko jipya la kuitwa Nakuja.

Ngoma ya Nakuja imekuwa ikidokezwa kwa muda mrefu sasa na Tommy Flavour kupitia akaunti yake ya Instagram. Hii ni ngoma ya kwanza kwa Tommy Flavour kwa mwaka huu wa 2023 pamoja na Marioo ambaye kwa sasa anatamba na The Kid You Know.

Nakuja ni ngoma ya Bongo Fleva yenye vionjo vya R&B na ndani yake, Tommy Flavour na Marioo wanatoa taarifa kwa wenzi wao kuwa wapo njiani wanakuja kwenye sehemu ambayo wameahidiana. Aidha kwa upande mwingine Tommy na Marioo wanatoa sifa kedekede kwa wenza wao.

Kwa mbali maudhui ya ngoma hii inafanana na ngoma ya Marlaw Pii Pii huku lyric video ya ngoma hiyo ambayo kwa sasa inapatikana Youtube inatukumbusha mbali kwenye video ya Hakuna a ya kwake Suma Lee.

Kutokana na ujumbe, melody kali pamoja na mashahiri mazuri ngoma hii ya Nakuja inatarajiwa kufanya vizuri huku ikiwa inatarajiwa kuwa tishio zaidi kwenye mtandao wa Tiktok na mitandao mingine.

https://www.youtube.com/watch?v=UviYi2oqHos

Leave your comment