Nyimbo Mpya: Dakota Tz Ft Mbosso 'Mungu Atusamehe' na Ngoma Zingine Mpya Za Singeli
2 February 2023
[Picha: Instagram]
Mwandishi: Charles Maganga
Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram
Kama unafuatilia muziki kutoka nchini Tanzania basi bila shaka utafahamu kwamba moja kati ya tanzu pendwa nchini humo ni muziki wa Singeli ambao unapambwa na wasanii tofauti tofauti Tanzania kama Meja Kunta, Dulla Makabila, Seneta Kilaka na wasanii wengine wengi ambao bila shaka kwa muziki wao wanaburudisha mno mashabiki.
Hizi hapa ni baadhi ya ngoma mpya na kali za singeli kutoka nchini Tanzania.
Mungu Atusamehe - Dakota TZ Ft Mbosso
Wazo zima la ngoma hii ni kuomba msamaha kwa Muumba juu ya makosa ambao binadamu wanafanya na bila shaka Dakota ameweza kuwasilisha wazo lake vizuri sana akitumia mashahiri makali kidogo pamoja na sauti kutokea fundi wa muziki kutokea WCB Wasafi Mbosso Khan.
Mchepuko - Seneta Kilaka
Seneta Kilaka hataki msongo wa mawazo kabisa na ndio maana kwenye ngoma yake mpya yake hii ya kuitwa Mchepuko, Seneta Kilaka anasema ni bora abaki kuwa mchepuko kwani hataki mawazo na changamoto zinazotokana na kubaki njia kuu.
Ruqaiya - Meja Kunta
Kwenye ngoma hii Meja Kunta anaturudisha kwenye enzi za Mamu ambapo anaonesha ufundi wake katika kutengeneza ngoma nzuri za mapenzi. Kwenye ngoma hii unakutana na Meja Kunta ambaye ametulia kisauti mpaka kimashahiri.
Njiwa - Chudy
Kila kitu kuhusu ngoma ya Njiwa ya kwake Chudy kinavutia kuanzia kiitikio chake mpaka ujumbe wa ngoma hii ambapo Chudy anaonesha mapenzi aliyonayo kwa mwenza wake. Hii ni moja kati ya ngoma bora za singeli kwa mwaka huu wa 2023.
Kwetu - Kadilida
Kadilida ameendelea kupeperusha bendera ya muziki wa singeli kupitia ngoma yake ya kuitwa Kwetu ambayo ndani yake anaelezea kuhusu maisha ya mtaani au sehemu ambayo yeye anatokea.
Leave your comment