Uhakiki Wa Vichwa vya Habari vya Magazeti ya Tanzania Leo 31- 01-2023

[Picha:Millard Ayo]

Mwandishi: Stellah Julius

Pakua na Kusoma matukio ya Magezitini ndani ya Mdundo

Mkurugenzi wa idara ya mawasiliano Ikulu Zuhura Yunus amesema ziara alizofanya Rais Samia nje ya Nchi zinatarajiwa kuleta matunda haswa kwa vijana na sekta ya kilimo nchini. Hayo aliyasema jana wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Ikulu juu ya ziara alizofanya Rias Samia Suluhu Hassan nje ya nchi. Mkurugenzi huyo wa mawasiliano alieza jinsi ambavyo Tanzania ilitumia fursa hiyo kwa kuwakaribisha wawekezaji nchini katika kuboresha kilimo kupitia miradi na Agenda mbalimbali. (Majira)

Kampuni ya uwekezaji ya International Holding Company (IHC) imetangaza kuwekeza Dola za kimarekani milioni 400 kwenye hisa za kampuni ya Adani Enterprises kupitia mfumo wa utendaji wa Rais Samia. Afisa mtendaji wa IHC bwana Syed Basar Shueb alisema hatua hiyo ya kununua hisa imekuja mara baada ya kuona fursa ya ukuaji wa kampuni ya Adani Enterprises. Uwekezaji wa kampuni ya IHC umekuja mara baada ya mikakati yake ya kuwekeza katika mabara ya Asia, Afrika, Amerika ya Kusini pamoja na Ulaya.(Majira)


Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Daniel Chongolo akiwa ziarani wilaya ya Kilosa mkoa wa Morogoro amesema Chama hicho kitaendelea kuhoji na kukagua miradi ya maendeleo kwa kuwa ni jukumu lao. Katika ziara hiyo pia alitoa maagizo kwa wizara ya Maliasili na utalii kulipa fidia kwa wananchi wenye mashamba 2005 ambao walifanyiwa uharibifu na tembo na pia akitaka vijiji 68 viwashiwe umeme kabla ya mwezi          April  mwaka     huu.  (Tanzanian Leo)

Gumzo limejiri nchini mara baada ya matokeo ya kidato cha nne kutangazwa na kuzuka kwa sintofahamu katika utata wa matokeo hayo. Baadhi ya mambo yaliyozua utata ni pamoja na ufungiwaji wa matokeo kwa wanafunzi wa shule ya Twibhoki ya mkoani Mara na kutoa matokeo ya mwanafunzi mmoja pekee, kuwepo kwa matokeo ya mwanafunzi wa kiume katika shule ya wasichana Musabe jijini Mwanza pamoja na kutokutajwa kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika matokeo au shule zilizofanya vizuri kama ilivyozoeleka. Katika matokeo hayo kati ya wanafunzi 333 waliofutiwa matokeo wanafunzi wanne waliandia lugha ya matusi. (Mwananchi)

Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko ya wakuu wa wilaya vigogo wawili wa Chama cha Walimu (CWT) hawakuhudhuria katika kiapao Cha nafasi zao hizo. Vigogo hao ni Leah Ulaya Rais wa Chama cha Walimu aliyeteuliwa katika wilaya ya Mbogwe pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Japhet Maganga aliyeteuliwa katika wilaya ya Kyerwa. Baada ya ya kushindwa kutaja sababu za kutokutaka kuapishwa Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Bwana Maganga alihojiwa na askari wa jeshi la polisi na alipofika mbele za waandishi wa habari hakusema chochote na taarifa zinasema ya kuwa watendaji hao wa Chama cha Walimu walimtaka Rais Samia atengue uteuzi wao na kuchagua watumishi wengine. (Mwananchi)

Watendaji wa serikali wameingia matatani mara baada ya kuhusika na vitendo vya rushwa kutoka katika mifugo yenye wastani wa kuwa 135 iliyokamatwa hifadhi ya Ruaha huku hakimu akiingia mitini wakati alipotakiwa kufuatilia kesi ya mifugo hiyo. Pia katika sakata hilo kiongozi wa Chama kimoja cha siasa aliyefahamika kwa jina la Kayumle Maungurusa alitajwa kukusanya pesa kwa wamiliki wa mifugo Mahakimu wasio waaminifu katika kesi. (Jamvi la habari)

Leave your comment