Nyimbo Mpya: Aslay 'Inauma', Nuh Mziwanda ' Nikizipata' Na Ngoma Zingine Mpya Tanzania Wiki Hii

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Maua Sama Ndani Ya Mdundo

Wasanii kutoka Tanzania wanajulikana kwa vitu vingi na moja kati ya vitu hivyo ni pamoja na kila wiki kuburudisha mashabiki zao kwa kuachia ngoma mpya ambazo zimelenga kukuza na kuchangamsha kiwanda cha muziki Tanzania.

Wiki hii wasanii kama Maua Sama, Aslay, Dayoo, Lord Eyez na wengineo wengi wameweza kutuletea ngoma mbalimbali kwe mitindo tofauti tofauti kama Amapiano, Bongo Fleva, Bongo Hip Hop na mengineyo mengi. Hizi hapa ni ngoma mpya Tanzania wiki hii.

Mr DJ - Maua Sama.

Katika harakati zake za kuitangaza albamu yake ya Love Waves, Maua Sama wiki hii amewashangaza wengi kwenye Bongo Fleva baada ya kuachia "Mr DJ" ngoma ambayo ndani yake, Maua Sama anamnanga na kumpa maneno ya Dharau mpenzi wake wa zamani. Humu ndani Maua Sama amefanya Amapiano ikiwa ni mara yake ya kwanza kufanya aina hiyo ya muziki.

https://www.youtube.com/watch?v=nYoWChyv4h0

 

Inauma - Aslay.

Baada ya kutupa Follow Me na Mozzah wiki  chache zilizopita, Aslay amerudi tena na Inauma. Kwenye Inauma, Aslay anamkumbuka mpenzi wake wa zamani ambaye kwa sasa yupo na mahusiano mengine. Ngoma hii inatukumbusha ngoma za zamani za Aslay kama Likizo, Hauna na Mhudumu.

https://www.youtube.com/watch?v=Z2LZsjrEgOc

 

Free Remix - Lord Eyez Ft Jay Moe & Nikki Mbishi

Kwa rapa Lord Eyez, dhana nzima ya kuwa huru ina maana kubwa sana na ndio maana akaamua kuwaita Jay Moe na Nikki Mbishi kwenye Free Remix. Humu ndani utapenda flows za Lord Eyez, michano ya Nikki Mbishi pamoja na midondoko ya Jay Moe na bila shaka wasanii hawa watatu wameweza kwa mara nyingine kupeperusha bendera ya Bongo Hip Hop nchini.

https://www.youtube.com/watch?v=Y20933NxFtA

 

Moyo - Dayoo

Ukiisikiliza Moyo ya kwake Dayoo utafahamu kwamba kuna sehemu Dayoo anaelekea kimuziki na ni sehemu nzuri sana. Kwenye Moyo Dayoo anashukuru na kutoa heko kwa mpenzi wake ambaye alimvumilia kipindi akiwa hana kitu mpaka kuja kuwa mtu mwenye kitu na kwa mara nyingine kupitia wimbo huu Dayoo ameweza kuonesha mapenzi yake na Bongo Fleva

https://www.youtube.com/watch?v=bBhmskRFxHk

 

Nikizipata - Nuh Mziwanda

Kwenye mkwaju wake huu mpya Nuh Mziwanda anajipambanua na kuiambia Tanzania ni jinsi gani tabia yake itakavyokuwa  na mambo atakayoyafanya siku akija kupata pesa za kumtosha. Huu ni mradi wa pili kwa Nuh Mziwanda kwa mwaka huu wa 2023

https://www.youtube.com/watch?v=bQOx80e16zM

Leave your comment