Collabo Zinazosubiriwa Kwa Hamu Tanzania 2023

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Maua Sama Ndani Ya Mdundo

Tangu Bongo Fleva uanze kurindima mwishoni mwa miaka 90 suala la collabo yaani wasanii au zaidi kushirikiana limekuwa ni jambo la kawaida sana ambapo kwa mara wasanii kutokea kiwanda hiki cha muziki Tanzania wamekuwa wakiunganisha nguvu ili kuwapelekea mashabiki kilicho bora.

Mwaka 2022, Marioo na Harmonize walituburudisha na "Naogopa", Diamond Na Zuchu walituletea "Mtasubiri" na ngoma nyingine nyingi ambazo zilipamba Bongo Fleva na kwa mwaka 2023 mambo yanatarajiwa kuwa sukari poa kwani kuna baadhi ya wasanii wamedokeza kuhusu collabo.

Zifuatazo ni baadhi ya collabo zinazotarajiwa kuachiwa Tanzania kwa mwaka 2023 :

Marioo & Diamond Platnumz

Hii ni moja ya collabo inayosubiriwa kwa hamu kubwa kwani kupitia mahojiano mengi anayoyafanya Marioo amekuwa akidokeza ujio wake.

Mara kwa mara Marioo amekuwa akidokeza, kuwa kupishana kwa ratiba ndio kitu kinachopelekea ngoma hii kuchelewa kutoka na kwa mwaka huu wa 2023 pengine Marioo anaweza akakata kiu ya mashabiki kwa kuachia ngoma hii.

Harmonize & Abigail Chams

Baada ya kushirikiana kwenye Closer na Leave Me Alone, hivi karibuni Harmonize amedokeza kwamba huenda ataachia ngoma nyingine na Abigail Chams hivi karibuni. Januari 10 mwaka huu Harmonize kupitia uwanja wake wa Instastory alichapisha video akiwa studio huku akidokeza kupitia caption kwamba atafanya na Abby Chams

Rosa Ree & Young Lunya

Hivi karibuni Rosa ree kupitia uwanja wake wa Instastory alichapisha video akiwa studio na Young Lunya na kisha kuandika "Young Lunya Tudrop Lini?" kitu ambacho kilipelekea mashabiki kusubiri kwa hamu ngoma hii kutoka kwa wakali hawa Hip Hop Tanzania kwa hamu sana.

Baba Levo & Diamond Platnumz

Kwa muda mrefu sasa, Baba Levo amekuwa akidokeza kuwa ngoma yake na Diamond Platnumz iko tayari na kwamba inatarajiwa kuachiwa hivi karibuni. Ikumbukwe kuwa Baba Levo na Diamond Platnumz walishawahi kushirikiana kwenye ngoma ya Shusha ambayo ilifanya vizuri.

Platform TZ & Rayvanny

Kupitia akaunti yake ya Instagram mwezi Desemba, msanii Platform TZ aliweka kionjo cha ngoma yake mpya na kisha kumtag Rayvanny ili afanye jambo na muda mchache baadae Rayvanny alijibu kwa kuonesha kuwa amekubaliana na jambo hilo

Leave your comment