Nyimbo Mpya:Aslay Aachia Ngoma Mpya "Inauma"

 

[Picha:Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Vanilla Ndani Ya Mdundo

Mwanamuziki kutokea lebo ya Rockstar Africa, Aslay ameendelea kupeperusha vyema bendera ya Bongo Fleva na hii ni baada ya hivi karibuni kuachia ngoma yake ya kuitwa Inauma.

Ngoma hii ya Inauma inakuja takriban mwezi mmoja tu tangu Aslay atikise Tanzania kwa ngoma zake mbili ambazo ni Moza pamoja na Follow Me ambayo amemshirikisha CEO wa Konde Gang, Harmonize. Aidha tangu aingie Rockstar Africa hii ni ngoma yake ya tatu kuachia ndani ya lebo hiyo.

Kama jina linavyojieleza, Inauma ni ngoma ambayo Aslay anaonesha kwa uwazi kabisa maumivu ambayo anapitia kwenye mapenzi. Kwenye Inauma, Aslay anaonesha wivu mkubwa alionao kwa mpenzi wake wa zamani ambaye kwa sasa anatamba akiwa na mpenzi mwingine.

Mashahiri ya Aslay kwenye Inauma yamejaa majuto, wivu na hisia kali ambazo zote kwa pamoja zinatukumbusha ngoma zake za zamani kama Likizo, Mhudumu pamoja na Hauna ngoma ambayo ilitoka takriban miaka 5 iliyopita.

Kufikia sasa bado Aslay hajaachia video ya Inauma lakini bila shaka atakata kiu ya mashabiki kwa kuachia video hiyo hivi karibuni.

Leave your comment