Free Download: Vanillah Music Arudi Kivingine  Na Video Ya "Nilimpenda Sana"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pakua na Kuskiza mziki wa Vanilla Ndani Ya Mdundo

Nguli wa muziki kutoka Tanzania, Vanillah Music kwa mara nyingine ameamua kukata kiu ya mashabiki zake baada ya kuachia kibao kipya kabisa cha kuitwa 'Nilimpenda Sana.'

Ngoma hii inakuja takriban miezi miwili tangu Vanillah Music ambaye alitangaza kujiunga na lebo ya Ali Kiba Kings Music mwishoni mwa mwaka jana, kuachia Unanisitiri Acoustic ambayo pia ilipokelewa vyema na mashabiki. Aidha Nilimpenda Sana ni video ya kwanza ya Vanillah Music kwa mwaka 2023.

Kwenye "Nilimpenda Sana" Vanillah Music anaugulia maumivu ya mapenzi ambapo kupitia ngoma hii Vanillah anahadithia jinsi alivyotendwa kimapenzi na binti ambaye yeye alikuwa akimpenda sana ambapo Vanillah anaeleza vitu ambavyo ana-miss kutoka kwa mpenzi wake huyo kama kupikiwa na mambo mengine mengi.

Ikumbukwe kuwa Nilimpenda Sana ni ngoma namba 4 kutoka kwenye EP ya Vanillah Music ya kuitwa Listen To Me.

https://www.youtube.com/watch?v=jebVjne_kO0

Leave your comment