Benpol Ataka Kumrudia Mpenzi Wake  Kwenye Ngoma Mpya "Wewe"

[Picha: Instagram]

Mwandishi: Charles Maganga

Pata Habari za Muziki na Mixtapes Kwenye Telegram

Kwa sasa nchini Tanzania Benpol ni moja kati ya wasanii wanaozungumziwa sana kutokana kauli yake hivi karibuni kuhusu ndoa yake ya zamani na mwanadada kutokea nchini Kenya Anerlisa.

Siku chache zilizopita akiwa anafanya mahojiano na Millard Ayo Benpol alinukuliwa akisema kuwa hakuwahi kufurahi ndoa yake na Anerlisa na kwamba yeye aliingia kwenye picha ili alete ukamilifu, kauli ambayo Anerlisa hakuipenda na kupitia Instastory yake alimuomba Ben Pol kuacha kumzungumzia.

Siku ya jana kupitia akaunti yake ya Instagram na Twitter Ben Pol alitolea ufafanuzi kuhusu sakata hilo ambapo aliomba radhi kwa matamshi yake na kusema kuwa hakuwa na nia mbaya ya kumuumiza yeyote.

Wakati haya yote yanaendelea, pia hivi karibuni Benpol aliachia ngoma yake ya "Wewe" ambayo ndani yake Ben Pol anaweka wazi kuwa yuko tayari kufanya chochote kumrudia mpenzi wake na ndani ya wimbo huu pia Benpol anaibua maswali mazito kuhusu nini hasa kilimfanya mpenzi wake huyo kuondoka kwani alijaribu kumpatia kila kitu.

Bila shaka Wewe ni moja kati ya ngoma bora sana kutoka kwa Benpol kutokana na uchaguzi bora wa maneno na mashairi, sauti nzuri pamoja na kiitikio ambacho kimejaa uraibu wa aina yake.

https://www.youtube.com/watch?v=1PtDJMuMWfA

Leave your comment